KAMBI YA MACHO CCBRT MBAGALA YAVUNA MAMIA YA WAKAZI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, March 29, 2026

KAMBI YA MACHO CCBRT MBAGALA YAVUNA MAMIA YA WAKAZI


NA MWANDISHI WETU

MAELFU ya wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake katika Manispaa ya Temeke, Jijini Dar es Salaam wamejitokeza kwa wingi kupima macho, kupata ushauri nasaha sambamba na kupata matibabu stahiki yalitolewa bure  Hospitali ya CCBRT jana.


Huduma hiyo ya macho na ushauri nasaha ni mpango endelevu wa Hospitali ya CCBRT kupambana na kutokomeza matatizo macho miongoni mwa Watanzania na kuzuia upofu usio wa lazima.


"Tumefurahishwa sana kwani watu wengi wamejitokeza kuja kupima macho, kupata ushauri nasaha na matibu bure,"Afisa Mkuu wa Maendeleo ya Jamii na Utafiti, Rhoda Ndakwe amesema na kuongeza kuwa uhitaji wa huduma hiyo ni mkubwa kutokana na idadi ya watu waliojitokeza.


Rhoda ambaye alimwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu, Brenda Msangi amesema CCBRT imejiwekea utaratibu wake kutoa huduma ya macho na ushauri ili kusaidia jamii kuepukana na ulemavu wa macho ikiwemo upofu.


Rhoda hakusita  kuwataja  Shirika la Christian Blind Mission (CBM) likishirikiana CCBRT kufanikisha zoezi hilo na kutoa wito kwa wadau wengi zaidi wajitokeze kudhamini zoezi kama hilo ili kuwafikia wahitaji wengi hapa nchini na kuwashukuru

 wafadhili mbalimbali wakiwemo CBM, Light For The World (LFTW).


“CCBRT kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tunalenga kutoa huduma  muhimu za macho ikiwemo kuwatambua mapema wenye ' Claucoma',' Cataract' na ndiyo maana tukaweka kambi kama hizi.


"Tunapenda kuwagundua mapema na kuhakikisha wanapata matibu mapema Alisema na kuongeza kuwa CCBRT ipo imara kuhakikisha inazuia ulemavu wa macho kwa Watanzania.


Hospitali ya CCBRT ni miongoni mwa hospitali chache hapa nchini zinazotoa huduma mbalimbali  za kibobezi zikiwemo   Huduma za macho, fistula, matibabu na usafishaji wa  figo, mifupa, huduma za uzazi na magonjwa ya wanawake, huduma za  upasuaji pamoja  radiolojia  na nyingine nyingi.





No comments:

Post a Comment