NAIBU WAZIRI WA NISHATI AANZA ZIARA YA KIKAZI KIGOMA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, March 5, 2026

NAIBU WAZIRI WA NISHATI AANZA ZIARA YA KIKAZI KIGOMA


NA MWANDISHI WETU

NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba ameanza ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Kigoma inayolenga kukagua miradi mbalimbali ya umeme ikiwemo mradi wa Malagarasi utakaozalisha megawati 49.5.


Kabla ya kuanza ziara hiyo amekutana Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dkt. Rashid  ChuaChua ambapo amepongeza Mkoa wa Kigoma kwa kusimamia miradi ya nishati kwa ufanisi.


Pia ametoa wito kwa viongozi wa Mkoa huo kuendelea kuweka mkazo katika kusukuma ajenda ya nishati safi ya kupikia na nishati safi kwa ujumla.


 Naye, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dkt. Rashid Chuachua amesema mkoa huo unaendelea kusimamia kwa ukaribu miradi ya nishati hususan ya umeme vitongojini.


Kwa upande wake,  Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigoma, Mganwa Nzota  amesema Mkoa wa Kigoma imekuwa ni mnufaika mkubwa wa mageuzi ya kinishati yanayoendelea kufanyika hasa baada ya mkoa huo kupata umeme wa gridi ambao umefanya umeme kuwa wa uhakika.






No comments:

Post a Comment