NA MWANDISHI WETU
NGOME ya Wanawake ya Chama Cha ACT - Wazalendo imezindua Mnara wa Kumbukumbu ya waliokufa Siku ya Oktoba 29, 2025.
Dorothy Temu Kiongozi wa Chama hicho, wakati wa kuzindua mnara huo, amesema wameamua kuutumia Mwezi Machi kufanya uzinduzi huo kutokana na kwamba mwezi kama huu, miaka kadhaa iliyopita Wanawake walikuwa Beijing China katika Mkutano, ulitoa fursa ya mapambano katika nyanja tofauti ikiwemo kiuchumi na kisiasa kwa mwanamke.
"Tumeamua kuuzindua Mnara huu wa mashujaa wetu waliokufa Oktoba 29, ili kuenzi harakati za mwanamke katika kudai haki za msingi, kisiasa na mengineyo.
"Taifa letu linahitaji uponyaji kutokana na yaliyotokea Oktoba 29, 2025 hivyo katika kuendeleza hayo tutahakikisha tutaembea nchi nzima kuzungumza na wanawake ili kuwa wamoja katika harakati mbalimbali kwa maslahi ya taifa," amesema.
Aliongeza kuwa kutokana na matukio yaliyotokea Oktoba 29, inatakiwa iundwe Tume Huru isiyopokea maagizo katika kukamilisha mchakato huo na itakayoketa takwimu sahihi ya waliopoteza maisha.
Naye Katibu wa Ngome ya Wanawake, Mkoa wa Dar es Salaam, Silvia Mathayo,amesema wanaungana na Ngome hiyo Taifa ili kuwakumbuka waliopoteza maisha siku ya Oktoba 29.
"Tunawasha mishumaa kuunga mkono sauti zinazopazwa na wanawake katika kupigania maslahi ya taifa letu na kulinda amani na tukio hili kutakuwa likifanyika kila mwaka, amesema.
Naye Naibu Katibu Mkuu, Ngome ya Wazee
Ali Mtumweni alisema wanaungana na Ngome ya Wanawake Taifa, kuzindua mnara huo ili kukumbuka hayo jambo linalosaidia kulinda misingi ya haki na amani.
"Tuna haki ya kuwaenzi kwa vitendo waliopoteza maisha ili kuhamasisha mchakato wa kupatikana Katiba mpya na uwepo wa Tume Huru ya Uchanguzi ya matukio ya Oktoba 29, "amesema.
.png)




No comments:
Post a Comment