SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUIWEZESHA OSHA ILI KULETA UFANISI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, April 29, 2026

SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUIWEZESHA OSHA ILI KULETA UFANISI


NA MWANDISHI WETU

SERIKALI imeahidi kuendelea kuiwezesha Wakala wa Usalama na Afya mahali pa Kazi(Osha), vitendea kazi ili kuleta ufanisi katika shughuli zake.


Ahadi imetolewa na Waziri wa Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus  Sangu, alipokuwa akifunga maadhimisho ya siku ya kimataifa ya usalama na afya mahali pa kazi,yanayofanyika viwanja vya Shule ya  Mjimwema,mkoani  Njombe


Waziri Sangu amesema wanayafanya hayo Osha ni taasisi muhimu katika kuleta ufanisi kwa wafanyakazi.


"Hivyo Serikali ina wajibu kuiwezesha Osha  vitendea kazi vyote muhimu ikiwemo magari na vifaa vya ukaguzi,"amesema Waziri Sangu.


Hata hivyo amesema  hadi sasa Serikali imeipatia Osha  magari 50 na vifaa vya ukaguzi vyenye thamani ya Shilingi bilioni saba.


Katika maadhimisho hayo pia Waziri Sangu ameziagiza Osha, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii( NSSF), kuhakikisha zinawabana waajiri ili wajisajili na kulipa madeni.


Akielezea Osha ,amesema licha ya kuwepo kwa waajiri 200,000 lakininwaliofikiwa na Osha hawazidi 100,000.


"Suala la kujisajili Osha ni takwa la kisheria na sio hiari hivyo kila mwajiri anapaswa kujisajili huko,"amesema.


Kwa upande wa WCF,amesema kuna sekta binafsi hawataki kuwasajili wafanyakazi wao katika mfuko huo na kutia siku 90 kufanya hivyonkabla hawajachukuliwa hatua za kisheria.


Naye  Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Tumaini Nyamhokya, katika usajili Osha , amesema kama kuna  wafanyakazi  hawalioni bango la Osha katika maeneo yao ya kazi wawape taarifa ili wahusika waweze kuchukuliwa sheria.


"Hawa Osha katika maeneo ya kazi ambayo wameshayasajili huwa wakiweka mabango yao,hivyo kama hulioni  ofisini kwako taarifa ili tuweze kuchukua hatua,"amesema Nyamhokya.


Awali  Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usalama na afya  Mahala pa Kazi(Osha), Khadija Mwenda, amesema katika maadhimisho hayo wameweza kuwafikia wajasiriamali 6101 na maofisa usafirishaji 300 na kuwapa vifaa kinga yote ikiwa kuhamasisha uwepo wa mazingira salama.


Katika ahadi yake,Khadija amesema wataendelea kuhimiza,kushauri kuhusiana na masuala ya afya na usalama mahali pa kazi kwani kutasidia kuokoa fedha za serikali na kuleta uvumilivu katika mifuko ya wafanyakazi.





No comments:

Post a Comment