WILAYA YA ILALA YAFANYA VIZURI MBIO ZA MWENGE UHURU 2026 - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, April 13, 2026

WILAYA YA ILALA YAFANYA VIZURI MBIO ZA MWENGE UHURU 2026


MWENGE wa Uhuru 2026 umeanza kukimbizwa katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo katika Wilaya ya Ilala miradi 7 yenye thamani *52,088,900,245.72* imepitishwa na Mwenge wa Uhuru hakuna mradi uliokataliwa.


Aidha katika miradi hiyo Mwenge wa Uhuru  umetembelea, umekagua, kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali  ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa kitega uchumi cha DDC Kariakoo, ujenzi wa barabara ya lami mtaa wa Lindi, ujenzi wa kisima cha Ilala kota, ujenzi wa kituo cha afya Mchikichini, ujenzi wa shule mpya ya sekondari kitunda relini, ujenzi wa kituo cha polisi Bonyokwa na Kikundi cha vijana Fighter wanaojishugulisha na usafirishaji wa abiria kwa kutumia pikipiki.  


Mwenge wa Uhuru 2026 leo April 14,  unaendelea Wilaya Kigamboni ambapo utatembelea, utakagua, kuweka Jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.





No comments:

Post a Comment