NAIBU MEYA DAR- MADIWANI PELEKENI VIJANA CHUO CHA FURAHIKA WAKAPATE MAFUNZO YA UFUNDI BURE - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, May 3, 2026

NAIBU MEYA DAR- MADIWANI PELEKENI VIJANA CHUO CHA FURAHIKA WAKAPATE MAFUNZO YA UFUNDI BURE



NA MWANDISHI WETU

NAIBU Mstahiki Meya jijini Dar es Salaam John Ryoba  ametoa wito kwa madiwani kutumia fursa ya uwepo wa Chuoni Cha Furahika kupeleka vijana kwa ajili ya kupata mafunzo ya ufundi bure.


Akizungumza katika mahafali yalifanyika mwishoni mwa wiki ,  amesema chuo hicho ni mkombozi kwa vijana waliokatisha masomo au kuishia kidato cha nne kutokana na changamoto mbalimbali 


"Hiki chuo cha kipekee kutokana kutoa mafunzo ya ufundi bure ili kuwasadia vijana kupata ujuzi wa fani mbalimbali, hivyo natoa wito Kwa madiwani wa Dar es Salaam na nchi nzima kuhakikisha wanaketa vijana wenye mazingira magumu wapate elimu ya ufundi utakaowakwamua katika maisha yao, binafsi katika Kata Yangu ya Kinyerezi nitaanza na wanafunzi 30," amesema.



 Ameongeza kila diwani popote alipo akileta wanafunzi hapa atakuwa anaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika harakati za kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya vijana wa Kitanzania.


Katika hatua nyingine Naibu Mstahiki Meya jijini Dar es Salaam ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kinyerezi ametoa nafasi ya mwanafunzi mmoja kumpa ajira katika na kumlipia Ada mwanafunzi mwingine.


Pia amewasisitiza wanahitimu hao kujiendeleza zaidi kielimu kufikia ndoto kubwa katika maisha yao.


"Rais wa zamani wa Afrika Kusini hayati Nelson Mandela enzi za uhai wake  alisema kuwa silaha pekee ya kupambana na umasikini ni kuwa na elimu hivyo licha ya kuhitimu masomo yenu endeleeni kujiendeleza ili mfikie ndoto za juu zaidi katika maisha yenu, amesema.


Naye Mirambo Shabani ambaye ni Mwakilishi wa Ofisi ya Mbunge Jimbo la Ukonga,  ... amesema kuhudhuria mahafali hayo yamempa  faraja kwa ameojionea vijana wanaomaliza wakiwa tayari kwenda kukitumikia taifa kutokana na ujuzi ambao wamepata katika chuo hicho.


"Unajua ukimpa mtu samaki hutakuwa ujasaidia ila ukimpa ndoani utakuwa umesadia katika maisha yake yote, hivyo chuo hiki kutoa mafunzo ya fani mbambali bure ni dhahiri kinawakomboa vijana wengi wa kitanzania katika kuanzisha safari yao maisha kwa kuachana na utegemezi," amesema.


Awali Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. David Msuya aliwakumbusha wahitimu hao huko wanapokwenda kuachana na tabia hovu ikiwemo ya wizi, uvivu na uasherati.

"Huko mnapokwenda kafanyeni kazi achaneni na tabia mbaya za uzinzi, wizi kwani mkiwa na tabia hizo kazi zitawashinda na mtarudi mtaani na kuwa ombaomba," amesema.








No comments:

Post a Comment