DKT MIGIRO, BALOZI UINGEREZA NCHINI TANZANIA WAJADILI USHIRIKIANO MAENDELEO, DIRA 2050 - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, June 5, 2026

DKT MIGIRO, BALOZI UINGEREZA NCHINI TANZANIA WAJADILI USHIRIKIANO MAENDELEO, DIRA 2050


NA MWANDISHI WETU

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Asha-Rose Migiro, leo Ijumaa Juni 5,2026 amefanya mazungumzo na Marianne Young, Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, katika Makao Makuu ya CCM, Dodoma.


Mazungumzo hayo yalihusu maeneo ya ushirikiano wa maendeleo kati ya Tanzania na Uingereza, kwa kuzingatia vipaumbele vilivyobainishwa katika Ilani ya CCM ya Uchaguzi ya mwaka 2025–2030, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 pamoja na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).


Viongozi hao walijadili fursa za kuendeleza ushirikiano kwenye maendeleo ya kijamii na kiuchumi, hususan katika kuwawezesha vijana na wanawake kupitia elimu, ujuzi, ubunifu na uwekezaji.


CCM inaendelea kuthamini ushirikiano wa kimataifa unaochangia maendeleo endelevu na ustawi wa wananchi wa Tanzania.




No comments:

Post a Comment