Jeshi la Polisi Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo (STPU) kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja kwa kosa la kutorosha Ngo'mbe 38 kwenda Nchi jirani kwa njia ya magendo.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kikosi hicho Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Simon Pasua leo Juni 16 ,2026 ambapo amesema kuwa mtuhumiwa huyo amekamatwa katika Kijiji cha Landarai, Kata ya Longido, Wilaya ya Longido, Mkoani Arusha katika oparesheni maalumu ambayo inafanywa na Kikosi hicho kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Kamanda Pasua amesema kuwa uchunguzi wa tukio hilo unaendelea kwa taratibu nyingine za kisheria, ambapo amewataka Wafugaji na wafanyabiashara wa mifugo nchini kuwa wazalendo kwa kufuata taratibu za kisheria katika usafirishaji wa mifugo nje ya nchi kwa kuwakatia vibali na kulipia ushuru kutoka kwa mamlaka husika.







No comments:
Post a Comment