OFISI YA WAZIRI MKUU YAFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU TAWALA MWANZA MASUALA YA USIMAMIZI MAAFA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, June 4, 2026

OFISI YA WAZIRI MKUU YAFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU TAWALA MWANZA MASUALA YA USIMAMIZI MAAFA


NA MWANDISHI WETU, MWANZA


KAIMU Katibu Tawala wa Mkoa Mwanza Henry Mwaijega amekutana na kufanya mazungumzo timu ya Idara ya Usimamizi wa Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu walipomtembelea ofisini kwake leo 04 Juni, 2026 Jijini Mwanza.


Timu hiyo ipo mkoani Mwanza kwa lengo la kuongoza mafunzo ya usimamizi wa maafa kwa Kamati za Usimamizi wa Maafa mkoa pamoja na wadau mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha utayari, uratibu na uwezo wa kukabiliana na majanga katika ngazi ya mkoa.


Pamoja na mafunzo hayo, wanatarajia kuzindua Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura cha Mkoa wa Mwanza 05 juni, 2026.








No comments:

Post a Comment