NA MWANDISHI WETU, KIBAHA
NAIBU Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana, Dk Kedmon Mapana amesema vijana kuwa na ujuzi na mtaji ni suluhisho la kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050.
Ameyasema hayo Mjini Kibaha kwenye Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere wakati akifungua kambi ya Vijana Uchumi Challenge.
Mapana amesema kuwa Waziri wa Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Joel Nanauka alizindua shindano la vijana kwa ajili ya kuwawezesha vijana nchini Tanzania kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi na ubunifu.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya Vijana Uchumi Challenge Joseph Malecela amesema kuwa jumla ya mawazo zaidi ya 7,000 ya vijana kote nchini yaliwasilishwa na kuchujwa na kubaki 100 ambayo yatashindanishwa kupata mshindi.
Malecela amesema kuwa washiriki hao 100 ambao wameingia kambini kwenye Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere watachujwa na majaji wabobezi wa masuala ya uchumi na fedha na kubaki 30 na baadaye 10.
Amesema kuwa washindi 10 watakwenda kwenye kilele kitakachofanyika Jijini Dar es Salam Julai 6 ambapo mshindi atapata kiasi cha shilingi milioni 50 huku wapili akijinyakulia shilingi milioni 20 na watatu milioni 10 ambapo vijana wanaoshiriki ni wenye umri chini ya miaka 35.





No comments:
Post a Comment