WAZIRI WA ULINZI DKT. NYANSAHO ATEMBELEA BANDA LA TANESCO MAONESHO YA SABASABA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, July 6, 2026

WAZIRI WA ULINZI DKT. NYANSAHO ATEMBELEA BANDA LA TANESCO MAONESHO YA SABASABA


NA MWANDISHI WETU


WAZIRI  wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho, leo Julai 06, 2026  ametembelea Banda la TANESCO katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) na kujionea ubunifu wa kidijitali unaolenga  kuongeza thamani ya matumizi ya nishati ya umeme kwa wananchi. 


Dkt Nyansaho ameshuhudia maendeleo ya Teknolojia ya nishati safi ya umeme katika vyombo vya usafiri, matumizi ya luku janja na teknolojia ya Nyumba Janja kwa maana ya (Smart House), inayomuwezesha mwananchi kudhibiti matumizi ya vifaa vya umeme kwa urahisi, kuongeza usalama wa nyumba na kufanya matumizi sahihi na yenye ufanisi  ya umeme.





No comments:

Post a Comment