Mbunge wa Viti Maalum Mkoa Wa Ruvuma, Mariam Madalu Nyoka akishangilia baada ya kukabidhi misaada mbalimbali wilayani Mbinga.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Ruvuma, Eliza Ngongi (watatu kushoto) akiwa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma, Mariam Madalu Nyoka (Mwenye miwani) na wa kwanza kutoka kushoto ni Katibu wa UWT Mkoa, Rehema Hosea.
Choo cha matundu sita ambacho kimejengwa na kukabidhiwa kwa wananchi na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma, Mariam Madalu Nyoka.
NA STEPHANO MANGO,MBINGA
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Mbinga kimetoa pongezi za dhati kwa, Mariam Madalu Nyoka, Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Ruvuma kwa kujenga choo cha kisasa chenye Matundu sita, matatu kwa wanaume na matatu kwa wanawake pia amekabidhi vifaa vya kutunzia maji na usafi kama ndoo na majaba vyenye thamani ya zaidi ya Tsh milion 10.2.
Akitoa tamko hilo Katibu wa Siasa na Uenezi, Donbosco Mkandawile amesema kuwa, Mariam Nyoka pia amekabidhi muziki ambao utatumiwa na kilabu cha Manzese ili kuepusha wajasiriamali wa pombe kutumia fedha nyingi kukodi mziki jambo ambalo lilikuwa linapunguza faida waliyokuwa wanaitarajia katika biashara hiyo muhimu ambayo inawasaidia wajasiriamali hao kukidhi mahitaji yao.
Mkandawile amesema kuwa CCM Wilaya ya Mbinga kinampongeza Mbunge kwa uchapakazi wake na michango yake ya hali na mali katika kutatua changamoto za wananchi wilayani humo na Mkoa kwa ujumla ambapo ndani ya muda mfupi ameweza kugusa maisha ya wajasiriamali, wagonjwa hospitali ya Mbuyula, Watoto yatima wa Kituo cha Masista Lusonga, Ujenzi wa Ofisi na mambo mengine
Aidha CCM kinampongeza kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM kikamilifu jambo linaloakisi shabaha ya CCM na kusaidia Serikali kuwa karibu na wananchi.
Alisema kuwa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mbinga kinatoa wito kwa viongozi wa ngazi zote kuendelea kutekeleza wajibu zao ili kutatua changamoto za wananchi wanaowaongoza kwa wakati.
Naye Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mbinga, Grace Millinga, amesema kutekelezwa kwa ahadi ambayo aliitoa Mbunge Nyoka kumeziokoa kura za CCM kutokana na umuhimu wa eneo hilo
Ameongeza kuwa eneo hilo ambapo kimejengwa choo lina mkusanyiko wa wapiga kura wengi ambao ndio waamuzi katika chaguzi za Mbinga hivyo kitendo cha kujenga choo bora katika eneo hilo kutarahisisha chaguzi zijazo
Kwa upande wake Mbunge Nyoka amesema kuwa ndani ya miezi tatu toka Mei hadi Agosti mwaka huu kwa Wilaya ya Mbinga tu ametumia jumla ya fedha milioni 24,573,000. Kwa ajiri ya kutoa misaada mbalimbali
Ameongeza kuwa pamoja na kukijenga choo hicho na kukikabidhi kwa wajasiliamali ambao wanafanya shughuli zao kwenye soko hilo pia amefanikiwa kununua geti la Kituo cha Watoto Yatima, St. Vicent Mbinga lenye thamani ya milion mbili.
Nyoka ameongeza kuwa watoto wa kituo hicho pia amefanikiwa kuwapatia mahitaji mbalimbali ikiwemo mablanket 70, mashuka 45, sabuni, mafuta sukari kg.50, sabuni katon tatu na Baby Shoo tano.
Amefafanua kuwa kwa upande wa wajasiriamali wajane (Waviu) aliwapatia mtaji wa mahindi wa milioni mbili, pia alichangia ujenzi wa Ofisi ya CCM Wilaya Mbinga, Cement mifuko 100 yenye thamani ya 1,700,000,
Katika kuendelea kuwainua wajasiriamali wadogo wenye mitaji chini ya 5000, aliwaongezea mtaji kila mmoja 15,000 idadi yao ni 72 ambapo jumla ya milioni 1,080,000, aliwapatia
Aidha ametoa viti mwendo kwa watu wenye ulemavu viwili , mashuka ya Wagonjwa 40, mashine za kupima presha mbili, kupima sukari mashine mbili, neti za vitanda vya wagonjwa 30 katika Hospitari ya Mbuyula Mbinga na kuwezesha vikundi saba vya kilimo cha maharage, mahindi na wahoka mikate kila kimoja kilipewa shilingi 500,000 na kufanya jumla ya milioni 3,500,000./=
No comments:
Post a Comment