Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan (watatu kushoto) kwa pamoja na Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya
CRDB Bank Foundation, Martin Warioba (kushoto) wakifanya tukio la uzinduzi wa
ujenzi wa soko la kisasa la CRDB Kizimkazi Dimbani linalojengwa kwa ufadhili wa
Taasisi ya CRDB Bank Foundation, unaonatarajia kugharimu takribani Shilingi
Bilioni Mbili hadi kukamilika kwake. hafla hiyo ambayo ni sehemu
ya shamrashamra za kuelekea kilele cha Tamasha la Kizimkazi, imefanyika
leo Agosti 29, 2023, Kizimkazi mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan (watatu kushoto) kwa pamoja na Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya
CRDB Bank Foundation, Martin Warioba (kushoto) wakifanya tukio la uzinduzi wa
ujenzi wa soko la kisasa la CRDB Kizimkazi Dimbani linalojengwa kwa ufadhili wa
Taasisi ya CRDB Bank Foundation, unaonatarajia kugharimu takribani Shilingi
Bilioni Mbili hadi kukamilika kwake. hafla hiyo ambayo ni sehemu
ya shamrashamra za kuelekea kilele cha Tamasha la Kizimkazi, imefanyika
leo Agosti 29, 2023, Kizimkazi mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa kuhusu ujenzi wa soko la kisasa la CRDB Kizimkazi Dimbani linalojengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya CRDB Bank Foundation, unaonatarajia kugharimu takribani Shilingi Bilioni Mbili hadi kukamilika kwake. hafla hiyo ambayo ni sehemu ya shamrashamra za kuelekea kilele cha Tamasha la Kizimkazi, imefanyika leo Agosti 29, 2023, Kizimkazi mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
............
KATIKA juhudi za kuendelea kuwezesha jamii
inayoizunguka kupitia sera yake ya uwekezaji kwa jamii, Benki ya CRDB kupitia
Tasisi yake ya CRDB Bank Foundation inatarajia kujenga soko la kisasa katika
Kijiji cha Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja visiwani Zanzibar. Hafla ya kuweka
jiwe la msingi la soko hilo imefanyika katika eneo la Kizimkazi Dimbani kama
sehemu ya shamra shamra za tamasha la Kizimkazi na kuhududhuriwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa soko hilo, Rais Dkt. Samia ameishukuru Benki ya CRDB kwa kukubali ombi la Mkoa wa Kusini kujenga soko hilo la kisasa ambalo litachochea maendeleo ya watu wa Kizimkazi na Mkoa wa Kusini Unguja kwa ujumla.
“Mwaka
jana kama mnakumbuka mlinipa kilio hiki cha soko la jamii ya Kizimkazi. Sasa
mimi nikalitupa Mkoa ambapo na wao wakalipeleka CRDB na leo wako hapa kwenye
field tayari kuweka jiwe la msingi na ujenzi unaendelea. Kwa hiyo tuwashukuru
sana CRDB kwa kutushika mkono katika hilo na haya ndo maendeleo ya Kusini
tuliyoyasema na ndo madhumuni ya tamasha letu hili la Kizimkazi” alisema Rais
Dkt. Samia.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema
kwa kutambua uchumi wa watu wa kusini unatemegea sana uvuvi, Benki chini ya
Taasisi yake ya CRDB Bank Foundation imeamua kuwekeza katika ujenzi wa soko la
kisasa ambalo litakwenda kuongeza thamani katika biashara kwa wakazi wa eneo la
Kizimkazi. Katika awamu ya kwanza ya ujenzi wa soko, Benki imetenga takribani
Shilingi Milioni 157.8 na tayari ujenzi wa sehemu ya kwanza tayari umeanza.
“Kwa muda mrefu Benki ya CRDB imekua mdau mkubwa wa maendeleo ya Kizimkazi kupitia tamasha la Kizimkazi ambapo hadi kufikia tamasha la mwaka huu, Benki ya CRDB imeshafanya uwekezaji wa takribani Shilingi Bilioni 1 na soko hili la kisasa la Samaki litaghrarimu zaidi ya Bilioni 2 hadi kukamilika kwake ambapo sehemu ya kwanza ya ujenzi itakamilika mnamo mwezi Oktoba 2023” amesema Nsekela.
Mbali
na utoaji wa huduma za fedha kwa wananchi wa pande zote mbili za Muungano, Benk
ya CRDB pia imekua ikitekeleza sera yake ya uwekezaji katika jamii katika pande
zote mbili. Sera hiyo ya uwekezaji katika jamii inaelekeza 1% ya faida
kurejeshwa katika jamii katika maeneo ya elimu, afya, mazingira na uwezeshaji
kwa wanawake na vijana.
“Mbali na ujenzi wa soko hili la kisasa, Benki kupitia taasisi yake ya CRDB Bank Foundation imeendelea na dhamira yake ya kuleta mageuzi katika mchezo wa Resi za Ngalawa ambapo katika tamasha la Kizimkazi la mwaka 2023, Benki imewekeza zaidi ya Milioni 119.5 katika mashindano ya Resi za Ngalawa ambazo ni sehemu ya Tamasha la Kizimkazi” aliongeza Nsekela. Mwaka 2021, Benki ya CRDB ilikua mdhamini kuu wa Tamasha la Kizimkazi kwa kugharamia tamasha lote asilimia kuanzia mafunzo kwa wajasiriamali, michezo, maonyesho ya wafanyabiashara hadi kilele cha tamasha. Mbali na hilo Benki ilifadhili ujenzi wa nyumba za madaktari na Ofisi ya Sheha.
Mwaka 2022, Benki ya CRDB ilijenga maabara ya Shule ya Sekondari ya Kizimkazi pamoja na kununua vifaa vyake vya maabara. Sambamba na hilo Benki ilifadhili michezo yote na zaidi kuleta mapinduzi katika mchezo wa Resi za Ngalawa ambapo uliweza kuvutia watu wengi zaidi na kutoa zawadi kubwa zilizoweza kubadili maisha ya wana Kizimkazi ikiwemo zawadi kubwa ya boti ya kisasa yenye thamani ya Shilingi Milioni 30 kwa mshindi.
No comments:
Post a Comment