Kova mgeni rasmi masumbwi ubingwa wa mabara - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, October 18, 2011

Kova mgeni rasmi masumbwi ubingwa wa mabara

Kova mgeni rasmi masumbwi ubingwa wa mabara
Na Asha Kigundula
MKUU wa Polisi Kanda Maalum ya Jiji la Dar es Salaam, Suleiman Kova, atakuwa mgeni rasmi katika pambano la Ngumi la Ubingwa wa Mabara wa UBO (UBO INTER-CONTINENTAL BANTAM WEIGHT CHAMPIONSHIP), kati ya bingwa mtetezi, Mbwana Matumla dhidi ya Francis Miyeyusho.
Pambano hilo la kukata na shoka linatarajiwa kupigwa Oktoba 30 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
.Akizungumzia pambano hilo, Kamanda Kova alisema kubwa zaidi lililomfanya akubali kuwa mgeni rasmi ni katika kunyanyua mchezo huo hapa nchini na kuoondoa makundi kwa vijana, ili wasiweze kufanya uhalifu, ikiwa ni pamoja na utumiaji wa dawa za kulevya.
"Nimekubali kuwa mgeni rasmi ili niwe mmoja wa wadau wanaopenda michezo iendelee, lengo likiwa ni kuondoa vijana wahalifu na makundi yasiyo salama ya vijana hapa nchini," alisema Kova.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Darworld Lindks ambao ndio waandaaji wa pambano hilo, Mohamed Bawazir, alisema maandalizi yake yanakwenda vizuri. Pambano hilo litakuwa la raundi 12, likitanguliwa na na mapambano matano ya utangulizi.
Alisema mapambano mengine ni kati ya Juma Fundi dhidi ya Fadhili Majia, Mohamed Matumla atapambana na Ramadhani Mashudu, wakati Issa Sewe atazipiga na Ramadhani Shauri.
Hassani Kidebe atazichapa na Deo Samweli na pambano la pekee la wanawake kati ya Asha Abubakari 'Asha Ngedele' dhidi ya Salma Kihombwa.
Katika pambano halo, kiingilio kitakuwa shilingi 10,000 kwa VIP, wakati viti vya kawaida sh 5000.

No comments:

Post a Comment