Msama awapiga tafu mawakala wa magazeti - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, October 20, 2011

Msama awapiga tafu mawakala wa magazeti

Na Asha Kigundula
KAMPUNI ya Udalali ya Msama Promotion kupitia gazeti la Dira linalomilikiwa na kampuni hiyo, jana imekabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh 800,000 kwa timu ya mawakala wa magazeti.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana katika hafla maalum ya kukabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya mkurugenzi wa kampuni hiyo, Alex Msama, Jimmy Charles alisema kuwa michezo ni ajira kwa vijana, hivyo kampuni yake imeamua kuzisaidia timu hizo ili kuinua na kuiendeleza.
Alisema kuwa huo ni mwanzo tu kwa kampuni yao kutoa vifaa vya michezo, ambapo wana mkakati wa kuendelea kutoa hadi kufikia kwenye timu kubwa kama Simba, Yanga na timu ya Taifa (Taifa Stars).

Charles alisema ni wajibu wa kila mmoja kusaidia sekta ya michezo hapa nchini kwa njia moja ama nyingine, hivyo kampuni yake itaendelea kutoa misada kwa timu zenye lengo la kufanya vizuri.
Nae nahodha wa timu hiyo, Hamisi Shabani alisema wamefurahishwa na hatua ya kampuni hiyo kwa kuwapa vifaa ambavyo ni changamoto kwao kuwa na timu nzuri na yenye ushindani.
Alisema wana mpango wa kuomba kushiriki katika mashindano ya NSSF kama watapata nafasi ya ombi lao kukubaliwa, na wao kushiriki sambamba na timu mbalimbali za kampuni za habari hapa nchini.
Vifaa vilivyotolewa na Msama ni jezi seti moja, mipira miwili na Soksi, vyote vikiwa na thamani ya sh.800,000.

No comments:

Post a Comment