Mkwasa ajifariji kipigo cha Simba - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, October 20, 2011

Mkwasa ajifariji kipigo cha Simba

Na Salome Millinga
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Ruvu Shooting, Charles Boniface Mkwasa amewapongeza wachezaji wake kwa kuonesha kiwamgo kikubwa kwenye mchezo wao waliocheza na Simba juzi.
Ruvu iliambulia kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu katika mchezo uliopigwa juzi kwenye Uwanja wa Azam uliopo Chamazi, Dar es Salaam..
Ruvu ambao walicheza vizuri katika kipindi cha kwanza walipoteza matumaini katika kipindi cha pili baada ya kuruhusu mabao kwa dakika za mwanza za kipindi hicho kutoka kwa Emmanuel Okwi na Haruna Moshi 'Boban'..
Akizungumza na Jambo Leo Dar es Salaam jana, Mkwasa alisema anachoshukuru ni kwamba timu yake imeweza kuonesha kuwa inafundishwa na kucheza vizuri katika mchezo huo, ingawa matokeo yamekuwa kikwazo kwao.
"Niliamua kuchezesha wachezaji wengi wa timu ya vijana (U 20) ili wazidi kupata uzoefu zaidi na kupata timu nzuri ya badaye, nashukuru hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na soka safi, tumefungwa kutokana na uzoefu tu," alisema Mkwasa.
Alisisitiza kuwa Simba ni timu kubwa hivyo wametumia uzoefu wao na kutumia makosa yao machache yaliyojitokeza katika safu ya ulinzi ambayo nayo ilikuwa makini kadiri ilivyoweza katika mchezo huo.
"Naamini nitafanya marekebisho katika makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo ule na kujipanga katika mchezo ujao na Moro United, kwa sababu itakuwa mechi ngumu kwetu pia," alisema Mkwasa.
Simba ambayo sasa ina pointi 24, imezidi kushikilia usukani wa ligi hiyo huku ikifuatiwa na maafande wa JKT Oljoro.

No comments:

Post a Comment