Na Hamisi Magendela
BONDIA Deo Njiku na Jonas Segu wanatarajia kupima uzito kesho katika Uwanja Jamhuri mkoani Morogoro kwa ajili ya pambano la uzito wa Kg 63 unaotambuliwa na Oganizeni ya Ngumi za kulipwa Tanzania (TPBO).
Akizunguza na Jambo Leo Dar es Salaam jana, Kocha wa ngumi nchini, Rajabu Mhamila 'Super D', alisema mabondia hao watapima uzito kesho ikiwa ni maandalizi ya mwisho kwa pambano linalotarajiwa kufanyika kesho kutwa mkoani humo.
"Mabondia wote wako katika hali nzuri na kesho watapima uzito katika Uwanja wa Jamhuri tayari kwa pambano hilo linalotarajiwa kuwa zuri na la kusisimua Oktoba 23, wote wamejiandaa kuonesha mchezo mzuri," alisema 'Super D'.
alisema mabondia wengine wanaotarajiwa kupima uzito ni pamoja na Cosmos Cheka, Idd Baba, Ramadhani Kido, Adola Mwambakifua, Seba Temba, Karage Suba.
Wengine ni pamoja na Juma Afande, Albert Mbena, Mkuyu Katoto, Yohana Mathayo na kwa upande wa Kick Boxer ni Hamisi Mwakinyo na Said Mbunda.
Katika pambano hilo, kocha huyo ataendelea kusambaza kwa wapenzi wa mchezo huo mafunzo ya ngumi ambayo yako katika mtindo wa DVD zenye mapambano mengi na mafunzo ya ngumi.
DVD hizo pia zinaonesha nyota wakubwa wa masumbwi kama akina Manny Pacquiao, De la Hoya, Floyd Mayweather, Ortiz na wengine wengi jinsi wanavyoumudu mchezo huo sambamba na maisha ya bondia Mtanzania anayeishi Marekani, Roger Mtagwa.
Thursday, October 20, 2011
New
Njiku, Segu kupimwa kesho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment