Azam yanoa koo kwa Polisi Dodoma - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, October 20, 2011

Azam yanoa koo kwa Polisi Dodoma

Na Hamisi Magendela
MICHUANO ya Ligi Kuu ya Vodacom inazidi kushika kasi ikiwa ukingoni mwa raundi ya kwanza na kila timu ikionesha upinzani mkubwa ilhali nyingine zikionesha udhahaifu.
Timu ya soka ya Azam leo inashuka katika Uwanja wake wa nyumbani Chamazi, Dar es Salaam katika mchezo wake dhidi ya Polisi Dodoma, ikiwa na kumbukumbu ya kufanya vizuri katika mchezo uliopita kwa kuitandika JKT Ruvu kwa mabao 2-0.
Azam ambayo kwa sasa ina pointi 18 ikiwa nafasi ya tatu, kama itashinda itajikita hadi nafasi ya pili, ambapo itakuwa imefikisha pointi 21 na kuipiku Oljoro yenye poiti 19.
Polisi Dodoma inayoshika nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, inatakiwa kujikakamua ili kushinda mchezo huo na kufanikisha kujiweka sawa kabla ya raundi hiyo kwisha.
Akizungumza na Jambo Leo Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Azam, Jaffar Idd, alisema vijana wao wako katika hali nzuri kwa mujibu wa kocha na waamini kuwa wataibuka na ushindi baada ya kupata muda mrefu wa kufanya mazoezi.
Aliongeza kuwa wachezaji wameahidi ushindi zaidi kuliko walioupata mbele ya JKT Ruvu, na tayari kocha wa timu hiyo, Stewart Hall amefanya marekebisho katika safu ya ushambuliaji.
Pia, taarifa kutoka ndani ya klabu ya Polisi Dodoma zinasema kuwa hawakuja Dar es Salaam kutalii, hivyo katika mchezo wao wa leo watafanya kila jitihada kucheza vizuri ili kuondoka na pointi tatu muhimu.

No comments:

Post a Comment