ABBY SKILLIZ: Msanii anayekuja upya kuwavaa chipukizi
. Hatamsahau Dully Sykes kwa kumuonesha njia
Na Hamisi Magendela
INAWEZEKA linapotajwa jina Abby Skiliz wako wanaoweza kudhani kuwa ni chipukizi anaechipukia katika medani ya muziki wa kizazi kipya nchini.
Kumbe ni msanii wa siku nyingi katika medani hiyo lakini kutokana na muziki kuwa na tabia ya kupanda na kushuka alipotea kabisa katika ya muziki na wengi walidhani kuwa ndiyo basi tena.
Katika hali isiyotarajiwa na wengi msanii huyo ameibuka upya akiwa na kazi inayofanya vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya na kusababisha werngi kuanza kufuata nyao zake.
Siku zote kimya kingi kinamshindo mkuu ndityo alivyoweza kujinasabu Abby Skiliz na kusema wakati wote alikuwa najipanga na kutafuta njia ya kutoka na kulishika soko la muziki ambalo linaonekana kuwa na ushindani mkubwa.
Msanii huyo ambaye ni mshabiki wa timu ya soka ya Simba anasema anajisikia faraja kuona wimbo wake wa Fara wa Mapenzi unafanya vizuri katika tasnia muziki wa kizazi kipya na kupokelewa vizuri na mashabiki.
"Sina kinyongo na watu ambao nahisi wanajaribu kufuata nyao zangu kwa mbali maana hiyo ndiyo changamoto katika muziki ama fani nyingine yoyote ninachotakiwa kufanya ni kukaza buti ili kurudisha adhi yangu ya awali," anasema Abby Skilliz.
Msanii huyo alianza harakati za muziki mwaka 2000 na baada ya kushawishiwa zaidi na Abdull Sykes 'Dully Sykes' na mwaka 2002 akafanikiwa kutoa wimbo wake wa kwanza uliofahamika kwa jina la Nilikupenda ambao uliweza kufanya vizuri katika anga za muziki wa kizazi kipya.
Anasema wimbo huo aliufanya katika studio ya G chini ya mtayarishaji Roy ambae kwa sasa ni marehemu na aliweza kumshirikisha vyema na Dully Sykes ambaye alinogesha vizuri katika kiitikio.
Nyota huo anasema baada ya kibao hicho kufanya vyema kilifuatiwa na kibao kingine kilichofahamika kwa jina la Mimi Na wewe alichoshirikiana na Henri Samil 'Mr Bluu' ambacho pia kiliweza kuvuta mashabiki wengi.
Utamu wa kutoa singo ulimzidi kumnogea na hatimae mwaka 2006 akaachia nyingine aliyoipa jina la Ngongongo aliomshirikisha na kipindi kifupi akaachia kibao kingine alikipa jina la Maria alioshirikiana vyema na Alli Kiba na Mr Bluu ambao pia uliweza kutikisa katika vituo mbalimbali vya redio.
Baada ya kutoa vibao hivyo aliakaa kimya kwa kipindi kirefu na wakati huo akiwa anatunga nyimbo mbalimbali ambazo hakuweza kuzipeka kwenye vyombo vya habari ili ziweze kusikika kupitia redio.
Anasema wakati akiwa kimya huku akijipanga namna ya kutoka ili kufanya vizuri katika tasnia ya muziki huo alifuatwa na uongozi wa kundi la njiwa dume na kutaka kufanya kazi ili aweze kurudi tena kama alivyokuwa awali.
Anaweka wazi kuwa baada ya majadaliano marefu akajipanga na kamua kutoka na kibao cha Fara Wa Mapenzi ambacho sasa kinafanya vizuri na kuwa gumzo katika tasnia hiyo ambacho aliweza kushirikiana vyema na mwana dada Zuu ambae aliweza kushiriki vyema katika wimbo huo.
Nyota huo mwenye mtoto mmoja anaitwa Shani mwenye umri wa miaka 3 ambaye amezaa na mwana dada aneitwa maria ambaye kwa sasa ni anafanya kazi katika Star Time, anasema amepata vikwazo vingi hadi kufikia katika hatua hiyo ikiwemo kukataliwa kuingia studio wakati anaanza muziki huo.
"Nilikuwa sikubaliki wakati naanza muziki lakini ujasili na kushauriwa na Dully Sykes ukanifanya nivumilie na kujipa moyo hadi nikaanza kuoneka na kupewa fulsa ambayo matunda yake yalianza kuonekana,"anasema Abby Skilliz.
Anasema uvumilivu wake wa kukubali kusumbuliwa wakati anaanza muziki kwa sasa anamalizia nyumba yake maeneo ya Pugu ambayo anatarajia kuishi baada ya kukamilika.
"Unajua mjini ukipata kibanda cha kuweka ubavu unashukuru mungu na kwa hatua niliyofikia mwenyezi Mungu apewe shuklani kubwa," anasema.
Hivyo anasema muziki unalipa kwa wanaofanikiwa na kikubwa anawaomba wasanii wenzake kujali familia zao na kutojisahau na kuhepuka vishawishi ambavyo vinaweza kuwasababisha kupata maradhi na kuangamia.
Pia amejipanga mwaka ujao wa kuachia nyimbo nyingine itakayofuana na albamu na kuwataka mashabiki kukaa tayari kuipokea.
Abby Skililz
Thursday, December 22, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment