Ngwasuma kuwakimbiza Arcade Des 23 - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, December 22, 2011

Ngwasuma kuwakimbiza Arcade Des 23

Na Asmah Mokiwa
BENDI ya muziki wa dansi nchini, FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma' inatarajiwa kufanya onesho la nguvu katika Ukumbi wa Arcade uliopo Mikocheni, Dar es Salaam, Desemba 23 mwaka huu.
Onesho hilo litapigwa kama utangulizi wa lile litakalopigwa katika Sikukuu ya Krismas Desemba 25, lililopangwa kufanyika katika Ukumbi wa New Msasani Club, Kinondoni.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa FM Academia, Kelvin Mkinga, alisema wamepanga kuwaburudisha mashabiki wao kwa kupiga nyimbo zao zote mpya.
Nyimbo mpya za bendi hiyo zitakazoimbwa katika usiku huo wa Arcade ni pamoja na Ndoa ya Kisasa, Fataki, Otilia, Dai Chako Ulaumiwe na Chuki ya Nini.
Mkinga alisema mpaka sasa, bendi hiyo imejianda kufanya vyema katika maonesho yao ya mwisho wa mwaka ikiwa pia ni maandalizi mazuri ya burudani za sikukuu za mwisho wa mwaka.
Alisema  wamejipanga imara kuhakikisha wanawapa  mambo mazuri mashabiki wao kwa kuziimba vyema nyimbo zao na kunengua kwa mikogo.

Alisema bendi hiyo iko imara na haina mpizani katika kipindi kirefu, hivyo wamewataka mashabiki wao wajitokeze kwa wingi kufurahia kazi za uhakika kutoka kwa wakali hao wanaotamba kama Wazee wa Ngwasuma.

No comments:

Post a Comment