Na Charity James
CHAMA cha Mpira wa Mikono Tanzania (TAHA) wamesema kushindwa kufanya vizuri kwa timu za hapa nyumbani kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Masharika kunatokana na maandalizi ya muda mfupi.
Akizungumza na Jambo Leo Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TAHA, Nicolaus Mihayo, alisema licha ya kuwa mwenyeji wa mashindano hayo, bado timu hazikuweza kufanya vizuri.
Mihayo alisema muda wa kujiandaa ulikuwa mfupi hasa pale mashindano yaliposimama kwa muda kupisha sherehe za miaka 50 ya Uhuru.
"Timu zetu zilijiandaa lakini si vile inavyotakiwa, ndio maana tumeshindwa kufanya vizuri katika michuano hii mikubwa Afria," alisema Mihayo.
Katibu huyo alisema licha ya kufanya vibaya, wanaipongeza timu ya Magereza wanawake kwa kushika nafasi ya pili katika michuano hiyo iliyokuwa migumu.
Mashindano hayo yalianza kutimua vumbi Desemba 11 katika Uwanja wa ndani wa Taifa, Dar es Salaam na kufikia tamati juzi katika uwanja huo huo.
Thursday, December 22, 2011
New
TAHA yatetea kuteleza kwao Klabu Bingwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment