Na Asmah Mokiwa
KOCHA wa timu ya taifa ya gofu raia wa Zimbabwe, Farayi Chitengwa, anatarajia kuondoka nchini Desemba 29, baada ya kumaliza mkataba wake wa kuitumikia timu hiyo.
Chitengwa aliingia mkataba wa miaka miwili wa kuifundisha timu hiyo ya taifa, ambapo aliingia mkataba huo Februari 2010, na unatarajiwa kumalizika Febuari mwakani.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Chitengwa, alisema ameamua kuondoka mapema baada ya kutokuwa na mashindano nchini hadi Febuari mwakani.
"Hakutakuwa na mashindano yoyote hadi Febuari mwakani ambapo mkataba wangu ndio unaisha, hivyo nimeamua kuondoka mapema na naamini niko sahihi," alisema Chitengwa.
Chitengwa aliliambia Jambo Leo Dar es Salaam jana kuwa yuko tayari kuifundisha timu hiyo na kuiletea mafanikio kama watamsainisha mkataba mwingine.
Alisema kwa sasa mchezo huo wa gofu umekua nchini ukilinganisha na miaka ya nyuma, ambapo Watanzania wachache ndio walikuwa wakishiriki mchezo huo.
Ndani ya miaka miwili aliyoitumikia kocha huyo, Tanzania imeweza kuonekana kwenye ramani ya gofu, kwa kufanikiwa kutwaa kombe katika mashindano ya Afrika Mashariki na Kati yaliyoshirikisha timu za wanawake. Na pia ilishika nafasi ya pili katika michuano ya Chalenji ya gofu ya Afrika Mashariki.
Thursday, December 22, 2011
New
Chitengwa amaliza muda wake, atimka
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment