Fidodido: Zao lingine kutoka Manzese - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, December 22, 2011

Fidodido: Zao lingine kutoka Manzese

Na Hamisi Magendela

MANZESE ni kitongoji chenye umaharufu mkubwa katika jiji la Dar es Salaam kutokana na mambo mbalimbali yalijitokeza na yanayondelea kutokea katika eneo hilo.

Vurugu nyingi za vijana nyanja mbalimbali zililikuwa zikifanywa katika eneo hilo na kuonekana kuwa sehemu ya changanyikeni na kila tabia iliyo nzuri na mbaya uonekana katika eneo hilo.

Kutokana na hali ya utukutu kwa baadhi ya vijana waliokuwa na wanaoishi katika eneo hilo, liliweza kuzalisha wanamichezo wa aina mbalimbali ambao kwa njia moja au nyingi waliweza kutoa taswila ya mafanikio katika nyanza hizo.

Tukizungumzia katika upande wa burudani, ukweli ni kwamba Manzese ni chimbuko la wanamuziki wa kizazi kipya wanaofanya vyema katika medani ya muziki huo nchini.

Hakuna aliyenashaka juu ya hilo kwa maana kuna makundi ya aina mbalimbali na wasanii mmojamoja lukuki wanaoendeleza sanaa ya muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva), ambao kwa umahiri wao wameweza kulitangaza vyema eneo la Manzese.

Ukizungumzia mmoja wa wamuziki wa kizazi kipya ambao wamo katika Kata ya Manzese, huwezi ukaacha kulitaja jina la Edward Paul ‘Eddo Star’ ama ‘Fidodido’, msanii anayejizolea sifa kwa kushirikishwa na wasanii mbalimbali wakiwemo makundi ya muziki huo.

 Inawezekana likawa jina geni miongoni mwa baadhi ya watu, lakini si jina geni kwa wafuatiliaji wa muziki wa kizazi kipya hasa katika miondoko ya ‘Ragga Dancehall’, ambaye anaonesha umahiri mkubwa katika upande huo wa muziki.

Msanii huyo yuko katikati ya makundi mawili ambayo anafanya kazi nayo pamoja na kutoa nyimbo kadhaa kwa ufanisi mkubwa bila ya kutetereka.

Makundi anayofanya nayo kazi ni pamoja na East Kama linaloongozwa na ‘Baharia’, ambalo linafanya vizuri na vibao mbalimbali kikiwemo Tunadanganyana, Kumpa Dumpa, Gamba Za Floor, na nyinginezo zikiwa zimetayarishwa katika studio ya Diefatelity chini ya mtayarishaji Mesen Selector.

Wakati huo huo, akiwa sambamba na kundi la Mexicana Lacavela na kushirikishwa katika vibao mbalimbali kama vile Ona inayotamba katika vituo mbalimbali ya redio, Cheche na Pitapitapiata.

Anasema kutokana na muziki wake kuwa wa Ragga, njia ya kufanikiwa ni nyeupe ukilinganisha na aina nyingine ya muziki wa kizazi kipya na kuamini siku moja atakuwa mwanamuziki wa kimataifa kama walivyokuwa wengine waliofikia hatua hiyo.

Fidodido, anasema ndoto yake kubwa ni kumiliki studio yake, kitu ambacho kitampa fulsa ya kuundeleza muziki wa Chakacha ‘Mnanda’, ambao anaamini ndiyo utakuwa mapinduzi ya katika tasnia ya muziki hapa nyumbani.

“Ukweli muziki wa mnanda ni muziki unaotoa sura ya kimapinduzi japo haupewi nafasi kubwa kwenye matamasha ya kitaifa kutokana na watu wengi kuhisi kuwa ni wa kihuni, lakini ujumbe wake una mafundisho makubwa katika jamii ya sasa na yajayo,” anasema Fidodido.

Kwa upande wake, tayari ameshafanya vibao kadhaa na vingine akitarajia kuviachia hivi karibuni, kazi ambazo amewashirikisha wasanii wakongwe ambao wanafanya vizuri katika tasnia ya muziki huo.

Anasema moja ya wimbo ambao ulikuwa ukifanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio ni Mchakamchaka, alioufanya katika studio ya Jahman.

Anasema baadhi ya nyimbo zinazotarajiwa kutoka hivi karibuni ni pamoja na Imejulikana, Noma na nyinginenezo, ambazo anatarajia kumshirikisha Ambwene Yessaya (AY) pamoja 20%, akiamini kuwa watafanikisha kazi zake kuwa bora zaidi.

Fidodido, anasema albamu yake inatarajiwa kuwa na nyimbo nane, zitakazosheheni ujumbe mzito ambao zitaweza kuwashtua wasanii wa kizazi kipya ambao wapo kwenye ‘Game’ muda mrefu.

Anasema anayazimikia mafaniko aliyonayo mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Joseph Mbilinyi, ambaye mashairi yake yataendelea kuwa somo katika jamii.

“Wakati mwingine nikiwa nasikiliza nyimbo za bwana mkuwa Sugu, huwa napata nguvu mpya ya kutunga mashairi mazito kutokana na hali ngumu ya maisha tunayokwenda nayo hivi sasa,” anasema.

Fidodido anawaomba mashabiki kukaa vizuri kupokea albamu yake pindi itakapokuwa tayari kwani ujumbe wa mashairi hayo yako katika mafundisho kulingana na ugumu wa maisha ya sasa kwa vijana.


Edward Paul 'Fidodido' kutoka kundi la muziki wa kizazi kipya Mexicana Lacavela akiwaka katika pozi.



No comments:

Post a Comment