Na Hamisi Magendela
RAIS wa Kundi la Mapacha Watatu, Kisso Muzuzu 'Ring Tune' anatarajia kuachia video ya wimbo wake mpya unaitwa Kungu aliyoshirikiana Kambi Kagiza 'Kambi.'
Akizungumza na Jambo Leo Dar es Salaam jana, Ring Tune, alisema video ya wimbo huo iko katika hatua za mwisho na wakati wowote ataisambaza kwenye vituo vya luninga.
"Nimejipanga kuwapa burudani mashabiki wangu kutokana na kufanya maandalizi ya kutosha ili kuweza kufanya kitu kinachoweza kuwa tofauti na watu wengine," alisema msanii huyo.
Ring Tune aliwaomba mashabiki kumpa ushirikiano wa kutosha ili aweza kufanya vizuri na kutimiza ndoto yake katika sanaa hiyo ya muziki.
Alisema katika video ya wimbo huo, msanii Kambi ameonesha uwezo mkubwa na kufanya kuwa tofauti na kazi za wasanii wengine.
Thursday, December 22, 2011
New
Kungu ya Ring Tune yakamilishwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment