Na Charity James
MSAANII wa muziki wa kizazi kipya kutoka katika Kundi la Tip Top Connection, Richard Ramadhan 'Richard Tunda' anatarajia kuachia wimbo mpya unaokwenda kwa jina la Mapenzi Yamenipiga Teke.
Akizungumza na Jambo Leo Dar es Salaam jana, Richard Tunda, alisema wimbo huo umetengenezwa katika studio ya kundi lao la Tip Top Connection inayo kwenda kwa jina la Dream Record na amemshirikisha Tunda Man.
Richard Tunda alisema wimbo huo tayari umekamilika, na wakati wowote mashabiki wake wa muziki wa kizazi kipya wakae mkao wa kula kuupokea katika vituo mbalimbali vya redio," alisema Richard Tunda.
Alisema mashabiki wasitegemee kazi mbaya kutoka kwake kwani anatarajia kibao hicho kuwa gumzo kama vibao vingine vilivyotangulia ambavyo vilifanikiwa kuteka mashabiki lukuki kikiwemo cha Basi Imba.
"Nilipofanya Basi Imba ilikuwa kama utani, lakini kwa sasa kinaonekana kuwa kilikuwa kibao kizuri, na hata hii ya Mapenzi Yamenipiga Teke itabamba bila shaka," alisema msanii huyo.
Thursday, December 22, 2011
New
Mapenzi yamempiga teke Richard
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment