Kwea Pipa aja kwa kusasambua - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, December 22, 2011

Kwea Pipa aja kwa kusasambua

Na Charity James
MSANII chipukizi wa muziki wa kizazi kipya nchini kutoka jumba la vipaji la Tanzania (THT) 'Kwea Pipa' amesema yupo mbioni kuachia video ya wimbo wake mpya unaoitwa 'Sasambua'.
Akizungumza na Jambo leo Dar es Salaam jana, Kwea Pipa alisema anatarajia kuachia video hiyo hivi karibuni ambayo imetayarishwa katika studio ya 'One' ye vidlab Production' chini ya mtayarishaji Gadau Jr.
Alisema wimbo huo umeimbwa kwa mahadhi ya mduara na umeanza kufanya vizuri katika maonesho mbalimbali ambayo msanii huyo amehudhuria kabla ya kurekodiwa na kufanyiwa video hiyo.
Akaongeza kwa kusema kuwa mtayarishaji wa kibao hicho alimsifu kijana huyo kwa kazi nzuri ambayo imeonesha kuwa ana uwezo wa kufanya kazi nyingi nzuri.
Kwea Pipa anawaomba mashabiki wa muziki wa kizazi kipwa wajiandae kupokea video ya wimbo huo kwani si muda mrefu atakuwa ameanza kuusambaza  katika luninga.

No comments:

Post a Comment