Na Hamisi Magendela
TIMU ya maafande wa Polisi Dodoma wanatarajia kuingia kambini baada ya Sikukuu ya Krismasi katika Uwanja wa Jamhuri kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu.
Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mkuu wa Polisi Dodoma, Leonald Kijagwa, alisema kwa sasa wanafanya mazoezi mepesi na baada ya sikukuu wataingia rasmi kambini kwa ajili ya kujiandaa kwa mzunguko wa pili wa ligi hiyo.
"Kwa sasa kikosi chetu kinafanya mazoezi mepesi kila siku asubuhi na jioni, lakini tunatarajia kuanza mazoezi kamili baada ya Sikukuu ya Krismasi na ratiba kamili itaanza rasmi," alisema Kijagwa.
Katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, timu hiyo haikufanya vizuri, hivyo katika mzunguko wa pili ambao ni wa lala salama inahitaji kufanya vyema ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kubaki kwenye msimu ujao wa ligi.
Kijagwa aliomba mashabiki wa timu hiyo kuwapa ushirikiano wa kutosha ili waweze kufanya vyema hatua hiyo ya lala salama na kuibakiza timu yao katika ligi hiyo.
Thursday, December 22, 2011
New
Polisi Dom yasubiri Krismasi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment