Mafuriko Dar yamsikitisha Dk Nchimbi - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, December 22, 2011

Mafuriko Dar yamsikitisha Dk Nchimbi

Na Asmah Mokiwa
WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Emmanuel Nchimbi, ametoa salamu za pole kwa waathirika wa mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam na kusababisha maafa katika baadhi ya maeneo ya jiji.
Akizungumza Dar es Salaam jana wakati akizindua kamati ya kukamilisha mchakato wa kupata vazi la Taifa, Dk Nchimbi alisema tatizo hilo la mafuriko ni janga la taifa zima, hivyo amesikitishwa kama kiongozi na tukio hilo.
Waziri huyo alitoa pole hiyo kwa wananchi waliopoteza ndugu zao na wengine kupotea kwa kusombwa na maji katika baadhi ya makazi ya watu yalioko mabondeni na karibu na mifereji mikubwa.
Mvua hizo zilianza kunyesha Desemba 20 na kusababisha mafuriko yaliyozaa vifo kwa watu kadhaa baada ya kusombwa na maji katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam.
Pia, zilisababisha maeneo mengi kuharibiwa kwa kusombwa na maji, ambapo miundombinu ya barabara imezidi kuharibiwa kutokana na madaraja muhimu kukatika na kufanya usafiri kuwa mgumu ndani ya Jiji la Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment