Basata yawataka wasanii kutafiti kwanza - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, December 23, 2011

Basata yawataka wasanii kutafiti kwanza

Na Mwandishi Wetu
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limeeleza kuwa, kuna kila sababu ya wasanii kufanya utafiti wa kina kabla ya kuandaa kazi zao ili zikubalike kwa walaji na si kujifurahisha wao wenyewe.
Wito huo umetolewa wiki hii na Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari BASATA, Godfrey Lebejo, wakati akizungumza na wadau wa sanaa katika Ukumbi wa BASATA, uliopo Ilala, Bungoni, kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa.

Lebejo alisema kuwa utafiti ni muhimu pale msanii anapotafuta wazo la kuandaa kazi ili kujua itakubalika kiasi gani kwa jamii na ni ujumbe wa namna gani unakusudiwa.
“Msanii lazima afanye utafiti ili ajue mlaji wa kazi yake anataka nini. Hauwezi kutengeneza kazi ili kujifurahisha mwenyewe mwisho wa siku mlaji ni jamii inayokuzunguka” alisema Lebejo.

No comments:

Post a Comment