Kwa hili ya Yanga mnastahili pongezi - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, December 23, 2011

Kwa hili ya Yanga mnastahili pongezi

Na Hamisi Magendela
JIJI la Dar es Salaam kwa sasa lipo katika majonzi makubwa kutokana na zaidi ya watu 24 kupoteza maisha kutokana na mafuriko makubwa yaliyotokea Desemba 20 mwaka huu.
Mbali ya kufariki kwa ndugu zetu hao, pia mafuriko hayo ambayo yametikiza Jiji la Dar es Salaam yamesababisha watu zaidi ya 5000 kukosa makazi kutokana na nyumba zao kuzingiwa maji.
Taarifa zilizopo zinaonesha zaidi ya watu 24 hadi jana jioni walikuwa wameripotiwa kufariki dunia kutokana na mafuriko hayo.Mungu azilaze roho za marehemu hao mahala pema peponi,Amina
Ni wakati mgumu kwa ndugu, jamaa na rafiki zetu ambao wamekumbwa na mafuriko hayo makubwa ambayo inaelezwa kuwa mvua iliyonyesha haijawahi kutokea kwa miaka mingi iliyopita.
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini imeweka wazi kuwa mara ya mwisho mvua kubwa ilinyesha mwaka 1954.Hivyo unaweza kuona tu kwa takwimu hiyo kwamba hali si shwari.Wakaenda mbali zaidi wakasema mvua iliyonyesha kwa siku moja inatosha kuwa mvua ya mwezi mzima.Mungu tunusuru waja wako.
Hata hivyo Watanzania kwa kuonesha umoja na mshikamano wao wameungana katika kusaidia kwa hali na mali kuhakikisha waathirika wa mafuriko hao ambao kwa sasa wapo katika maeneo maalumu wanapata msaada wa huduma muhimu.
Kutokana na upendo huo Klabu ya Yanga ya Dar es salaam ni moja kati ya waliojitokeza kusimama imara kuhakikisha nao wanakuwa sehemu ya Watanzania ambao wanasaidia waliokumbwa na mafuriko hayo.
Klabu ya Yanga katika kuhakikisha inasaidia waathirika hao imeamua kuchukua waathirika 400 kwa lengo la kuhakikisha wanapatiwa hifadhi ya muda katika jengo la Makao Makuu ya klabu hiyo.Yanga ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Upendo wa Yanga kwa ndugu zetu hao hakika unakumbusha wakati nchi yetu inapigania uhuru wake kwani jengo hilo ambalo leo linahifadhi waliokumbwa na mafuriko ndilo lilitumika katika harakati za kudai uhuru wetu.
Kufuatia kuguswa na tatizo hilo klabu hiyo ililazimika kufuta na kusitisha kwa muda baadhi ya programu zao na moja mchezo wa kirafiki wa kimataifa ambao ulitakiwa kufanyika leo dhidi ya Escom ya Malawi ambao wamesogeza mbele ambao unatarajiwa kufanyika Desemba 26 au 27 mwaka huu.
Hongereni Yanga kwa uthubutu huo ambao unastahili kuigwa wa Klabu nyingine ambao zinauwezo mkubwa wa kifedha kuliko nyinyi.
Nakubali usemi usema kutoa ni moyo usambe si utajili.... inshaala Mungu atawazidishia kwa hilo mlilolifanya kwa waathirika hao wa mafuriko.
Hakika mmeonesha utu wa kibinadamu ambayo inastahiri kuigwa na klabu nyingine za michezo ili kuonesha ushirikiano. kama kauri mbiu ya michezo inavyosema kuwa michezo ni ndugu.
Kwa maana kupitia michezo tunajenga udugu wa kusaidiana katika raha na shida, hivyo Klabu ya Yanga imeonesha kuimalisha udugu katika kuwasaidia waathirika katika kipindi hiki kigumu.
Naamini watawakumbuka milele na msaada wenu umewaweka katika ramani nyingine. Heko heko heko Yanga.
Hongereni sana. Waathirika hao hawana chakuwalipa naamini Mwenyezi Mungu ameliona hilo kwa jian lake atawapa kinachostahiri, hakika mmeonesha mfano wa kuigwa.
Watoto wadogo waliopatiwa hifadhi katika jengo lenu watatoka hapo na kitu kipya vichwani mwao na kamwe hatosahau katika maisha yao yote. hakika mmetukumbusha mwaka 1961.

No comments:

Post a Comment