Cheka amtahadharisha Nyilawila - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, December 23, 2011

Cheka amtahadharisha Nyilawila

Na Asmah Mokiwa
BINGWA wa Mabara katika masumbwi, Francis Cheka [SMG] amemtaka mpinzani wake Karama Nyilawila kusubiri kichapo katika pambano lao lisilokua na ubingwa litakalopigwa Januari 28 mwakani.
Mabondia hao wataingia ulingoni kupambana katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, mkoa ambao Cheka anaishi.
Cheka na Nyilawila hawajawahi kushikana katika mapambano yaliowahi kuandaliwa nchini, hivyo mashabiki wa masumbwi watafungua mwaka kwa kushuhudia pambano hilo la aina yake.
Akizungumza Dar es Salaam jana kuhusiana na pambano hilo litakalokuwa la raundi 10 na uzito wa kg 72, Cheka amemtaka mpinzani wake afanye mazoezi ya kutosha ili kumkabili.
Alisema mabondia wengine nchini wameshindwa kumpiga, hivyo awe makini la sivyo atachezea kichapo cha aina yake na kuweka historia nyingine katika masumbwi.
Katika pambano hilo kutakua na mapambano ya utangulizi, ambayo yatawakutanisha mabondia Maneno Osward (mtambo wa gongo) na Pasco Ndomba raundi nane uziti wa kg 75, Chaulembo Palasa na Deo Njiku kg 68.
Venance Mpoji naye atavaana na Ibrahim Clases kg 63, Anthon Mathias na Juma Afande kg 54 na pambano la mwisho kati ya Hassan Kidebe na Arbert Mbena kg 54 ambapo mapambano hayo yatakuwa ya raundi sita kila moja.

No comments:

Post a Comment