Na Hamisi Magendela
MSANII wa muziki wa kizazi ambaye yuko sanjari na sanaa ya uigizaji, Abbas Hamisi '20%', anatarajia kuchia filmu yake ya tatu Januari mwakani.
Msanii huyo alisema filamu hiyo inatarajiwa kuvutia zaidi ya iliyopita kutokana matayarisho yake kuwa makubwa ili kuweza kuteka mashabiki wa tasnia hiyo.
Akizungumza na gazeti hili jana, 20%, alisema filamu hiyo itajulikana kwa jina la Haki Iko Wapi, ambayo itakuwa na vionjo vya nyimbo zake na kuendena na matukio ya mashairi hayo.
"Filamu yangu itakuwa nzuri kutokana na kuipanga vyema na kurekebisha makosa ya awali ili iweze kupata mafanikio ya kutosha kuzidi uliyopita ambayo pia ilifanya vizuri.
"Filamu yangu ya kwanza niliipa jina la Furaha Iko Wapi, na ya sasa inaitwa Haki Iko Wapi, hivyo unaweza kuona tofauti iliopo, ninachoomba kwa mashabiki wangu kukaa tayari kuipokea kazi hiyo," alisema 20%.
Friday, December 23, 2011
New
20% sasa atafuta haki
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




No comments:
Post a Comment