Na Asha Kigundula
KUNDI la muziki wa mwambao la Jahazi Modern Taarab leo linafanya uzinduzi wa albamu yake ya Mpenzi Chocolate, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Akizungumza na Jambo Leo Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wake, Mzee Yusuf ‘Mfalme’, alisema maandalizi ya uzinduzi huo yamekamilika, na kilichobaki ni kuanza kwa onesho hilo.
Yusuph alisema mbali na uzinduzi wa albamu hiyo, siku hiyo, kundi lake la Jahazi Modern litasherehekea miaka sita tangu kuanzishwa kwake.
Alisema itakuwa siku maalum kwani hata kundi la Taarab Asilia, Nadi Ikhwan Safaa na msanii wa Bongo Fleva, 20% (Hamis Kinzasa) watakuwepo kusindikiza uzinduzi huo.
Alisema albamu hiyo itakuwa na nyimbo nne ambazo ni wimbo uliobeba jina la albamu wa ‘Mpenzi Chokolate’ ulioimbwa na Mzee Yusuph, Sina Muda huo’ (Leila Rashid), ‘Zibeni Njia’ (Khadija Yusuf) na ‘Full Shangwe’ (Prince Amigo).
"Ninaamini onesho litakuwa zuri sana kwangu na hata wale watakaotusindikiza katika uzinduzi wete, kila kitu kiko tayari na tutawassha moto kama ambao unafahamika kwa Jahazi," alisema Yusuph.
Friday, December 23, 2011
New
Mpenzi Chocolate ya Jahazi leo Diamond
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




No comments:
Post a Comment