BAADA ya kutamba na kibao kilichobeba jina la albamu ya pili ya Mida Ya Kazi, msanii Abrahaman Kassembe 'Dullayo', yuko mbioni kuachia kibao kingine Januari mwakani.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Dullayo alisema wimbo huo tayari umekamilika na Januari Mosi utaanza kusikika kwenye vituo mbalimbali vya redio.
"Daa..! Hiyo ngoma itakuwa kali kupita maelezo kutokana na kuandaliwa vyema kwenye studio ya Imotion, chini ya mtayarishaji mahiri, Kisaka," alijifaragua Dullayo.
Alisema wimbo huo ameupa jina la Nimeamua, ambao kutokana na ujumbe wake anaamini itafanya vyema katika ushindani wa nyimbo za kizazi kipya nchini.
Msanii huyo, awali aliweza kutamba na vibao kama vile Twende Na Mimi, Mida Ya Kazi, Naumia Roho na nyinginezo ambazo bado zinafanya vizuri na mashabiki kuziomba katika vipindi mbalimbali vya redio.
Amewatuliza mashabiki wake kuwa bado ana kazi nzuri na za kuburudisha wanazotakiwa kuzisikia kutoka kwake, hivyo waendelee kumpa sapoti katika kile anachokifanya.
![]() |
| Dullayo aikiwa katika pozi |





No comments:
Post a Comment