- Itazivuka Azam, Simba ikishinda 4-0 leo
Na Asha Kigundula
MABINGWA watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga, wanashuka dimbani leo kuivaa Mtibwa Sugar, katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga inatakiwa ishinde katika mchezo wa leo ili iweze kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wake, na kuifikia Simba ambayo iko kileleni kwa pointi tatu zaidi ya mabingwa hao.
Endapo itakubali sare ya aina yoyote ile, itakuwa imejiweka pabaya kutokana na kasi iliyokuwa nayo timu ya Azam FC, ambayo kwa sasa imeishusha Yanga kutoka nafasi ya pili katika msimamo mpaka ya tatu.
Simba ina pointi 34 kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ikifuatiwa na Azam FC, ambayo ushindi wake wa juzi umeifanya kufikisha pointi 32, mbili juu ya Yanga ambayo sasa iko katika nafasi ya tatu.
Yanga yenye pointi 31 ikishinda mchezo huo kwa idadi ndogo ya mabao itashika nafasi ya pili, endapo itashinda kwa zaidi ya mabao manne itakuwa imepanda mpaka nafasi ya kwanza na kuishusha Simba kutoka kileleni.
Mtibwa Sugar iliyopoteza mechi mbili, inataka kupata ushindi katika mchezo huo ugenini ili iweze kuondoa hali ya hofu kutoka kwa wapenzi wao, baada ya kufungwa katika mechi zake za mwanzo za mzunguko wa pili.
Katika mchezo wao wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1, mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Endapo timu hizo zitagawana pointi, Yanga itaendelea kukaa katika nafasi ya tatu kutokana na wingi wa mabao ya Azam ambayo ina pointi 32.
Mechi hiyo itachezeshwa na mwamuzi Ibrahim Kidiwa kutoka Tanga, wakati wasaidizi wake ni Michael Mkongwa kutoka Iringa na Kudura Omary wa Tanga. Kamishna wa mechi hiyo ni Mohamed Nyange kutoka Dodoma.
Katika mchezo huo pekee wa Ligi Kuu kwa siku ya leo, ambao utaanza saa 10:30 alasiri, kiingilio kitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B na sh. 15,000 VIP A.
Tuesday, February 7, 2012
New
Yanga yanusa harufu ya kileleni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




No comments:
Post a Comment