Kagera Sugar kumshitaki Swedi TFF - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, December 22, 2011

Kagera Sugar kumshitaki Swedi TFF

Na Hamisi Magendela
UONGOZI wa timu ya soka ya Kagera Sugar unajiandaa kumuadhibu mchezaji wake  Hussein sued kutokana na kutofika kwa muda kwenye kambi ya timu huyo.
Akizungumza na Jambo Leo kwa njia ya simu kutoka mkoani Kagera jana, Mratibu wa timu hiyo, Mohammed Hussein, alisema imekuwa ni kawaida kwa mchezaji huyo kuikacha timu hiyo mara kwa mara wanapotoka likizo na kuamua kuchelewa kwa sababu zisizo na uzito.
Alisema kutokana na sababu hiyo, wanatarajia kukaa Desemba 26 mwaka huu kujadiliana kwa pamoja na kulifikisha suala hilo katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ajili ya kumchukulia hatua zaidi za kinidhamu.
Aliongeza kuwa Swedi atakaa nje ya uwanja kwa kipindi chote cha mzunguko wa pili na kukosa haki zake stahili zilizoko kwenye klabu hiyo ikiwa ni kiasi cha fedha zake za usajili pamoja na mshahara.
"Ni kawaida yake kuikacha timu yetu hata msimu wa kwanza alifanya hivyo mara kadhaa na wakati mwingine tunamsikia akicheza ndondo katika timu moja ya Veterani ya Boko," alisema Hussein.
Pia, alisema mchezaji huo aliwahi kuwakacha wakati walipocheza na Moro United jijini Dar es Salaam na baadhi ya mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Alisema timu yoyote inayomtaka mchezaji huyo italazimika kufuata taratibu zote na kulipa gharama zao kwani bado ana mkataba na kikosi hicho.

No comments:

Post a Comment