Mbishi real kusambaza kazi zake mwenyewe - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, December 20, 2011

Mbishi real kusambaza kazi zake mwenyewe

Na Hamisi Magendela
KUTOKANA na kuonekana kunyonywa na baadhi ya wasambazi wa kazi za wasanii, msanii Fred Kaguo 'Mbishi
Real' yuko katika hatua za mwisho kusambaza mwenyewe
albamu yake.

Alibaisha hayo alipozungumza na gazeti hili na kuamini kuwa hatua yake ya kuisambaza mwenye albam yake
itakuwa ya mafanikio kutokana na tafiti alizofanya.

"Tayari nimezungumza na baadhi ya wateja wangu na wameonesha mwitikio mkubwa wa kununua kazi zangu
hivyo naamini nitafanya vizuri," alisema Mbishi Real.

Alisema lengo la kufanya hivyo limetokana na wasambazaji aliozungumza na kutaka albamu hiyo wa bei
raisi isiyomlipa.

Hivyo alisema ni vyema wasanii wakawa kitu kimoja kihakikisha wanasambaza kazi zao wenyewe na kuepuka
sualazima kuwatajirisha wasambazaji na wao kuendelea
kuwa masikini.

Alisema tayari ameshatoa kopi 30,000 za albamu hiyo inayoitwa Tozi wa mbagala yenye nyimbo 12, ikiwemo
Tozi wa Mbagala, Amebaka, Baba na Mama, Pombe,
Mama Poa na nyinginezo.

No comments:

Post a Comment