Na Hamisi Magendela
MSANII Ambwene Yesaya 'AY' amesema mafanikio aliyoyapata kupitia sanaa ya muziki alianzia kujitangaza Tanzania na kusambaa Afrika.
Akizungumza na Jambo Leo kabla ya kwenda Afrika Kusini kurekodi wimbo wake unaoitwa Part Zone alisema kujitangaza kwake nchini kilisaidia kutambulika nchini za nje na kupata mafanikio aliyonayo sasa.
"Ninachoweza kusema ni kwamba ni vyema wasanii wachanga wakaanzia kujitanga nyumbani ndiyo watafute njia za kutanua wigo wa kimuziki nje ya nchi," alisema AY.
Alisema kila kitu ni lazima kiwe na msingi wake ambao utaimaliza mwendelezo wa kazi nyingine zitakazomfanya akubalike nje ya nchini na kwa kujitangaza zaidi kupitia kazi mpya.
Hivyo aliwataka wasanii wajijengee misingi imara tangu awali itakayoweza kuhimili ushindani wa muziki wa kimataifa na wasanii wengine ambao wanafanya vyema duniani.
AY akitumbuiza jukwaani |
No comments:
Post a Comment