Na Hamisi Magendela
MSANII Joseph Lushahu 'Bwana Misosi' amesema wimbo wake wa Nakungoja hadi kukamilka kwake kwa upande wa audio na video umetumia shilingi Mil 1.5.
Akizumngumza na Jambo Leo, jana kwa njia ya simu akiwa jijini Tanga, Bwana misosi alisema anashukuru kwa kazi zake kumilika japo kulikuwa na changamoto nyingi.
"Kulikwa na changamoto nyingi ambazo kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu nimeweza kuzikabili na kazi yangu imekamilika na keshokutwa naanza kusamba katika vituo mbalimbali vya redio na luninga," alisema Bwana Misosi.
Bwana misosi amesema kuwa katika wimbo huo amemshirikisha msanii chipukiza anayeitwa Migigi ambaye amafanya vizuri katika mashaiti yake.
Alisema wimbo huo wenye mahadhi ya Raggae imetengenezwa katika studio ya Combination Sound chini ya Man Water wakati video imetengezwa na Bongo Land Picture.
Mkali huyo mwenye taaluma ya umeme alianza kutambulika katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya baada ya kuachia kibao chake kinachoitwa Nitoke Vipi.
![]() |
Joseph Lushahu Bwana 'Misosi'. |
No comments:
Post a Comment