Shindano mchezo wa Judo kuanza Keshokutwa
Na Hamisi Magendela
SHINDANO la mchezo wa Judo 'First Grand Slam National Judo Championship' yanaanza kutimua vumbi kwa siku mbili Mei 26 na 27 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Magendela Blog Dar es Salaam jana Mwenyekiti chama cha Judo Tanzania 'Jata' Halfa Kiumbemoto 'Chief Kiumbe' alisema maandalizi ya shindano hilo yamekamilika.
"Kila kitu kinakwenda sawa na wachezaji wachezaji wataanza kuwasili Hotelini Ijumaa kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya shindano hilo ambalo litaanza Jumamosi na kuisha Jumapili," alisema Chief Kiumbe.
Chief Kiumbe alisema Shindano hilo lilikuwa likifanyika nje ya nchi na sasa ni mara ya kwanza kufanyika nchini likiwa na lengo la kuinua na kuutangaza mchezo huo.
Alisema katika shindano hilo kutakuwa na upande wa Wanawake na Wanaume wakipigana katika uzito tofauti na wakianzia kilo 60, 66, 73, 81, 90 , 100 na kuendelea.
Aliongeza kuwa bingwa wa shindano hilo kwa upande wa Wanaume na Wanawake atajinyakulia dola za Marekani 600, mshindi wa pili dola 300 na mshindi wa tatu atajinyakulia dola 100.
Pia mchezaji bora atajinyakulia kitita cha dola za Marekani 1000 ambaye atapigana kwa kutozingatia uzito, kwa maana wa kila 60 anaweza kupigana mchezaji wa kila 100.
Tuesday, May 22, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment