- MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, May 22, 2012

Ligi ya Taifa ya TFF kuanza Mei 26
Na Asha Kigundula
LIGI ya soka ya Taifa inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 26 mwaka huu katika vituo vya Mara, Musoma, Mtwara na Kigoma.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema kuwa ligi hiyo itakuwa kwenye vituo vitatu.
Wambura alisema leo, Kamati ya Mashindano itakutana kujadili mambo mbalimbali yahusuyo mashindano hayo. Hadi kufikia jana, hakukuwa na pingamizi lolote la kupinga timu zilizoingia hatua hiyo.
Timu zinazoshiriki ligi hiyo ni mabingwa wa mikoa, ambao ni Ashanti United ya Ilala (Dar es Salaam), Aston Villa (Singida), Bandari FC (Kagera), CDA (Dodoma), Flamingo SC (Arusha), Forest FC ya Siha (Kilimanjaro), JKT Kanembwa (Kigoma), Korogwe United ya Korogwe (Tanga), Kurugenzi ya Mafinga (Iringa), Lindi SC (Lindi) na Majimaji (Tabora).

Mighty Elephant (Ruvuma), Mkamba Rangers ya Kilombero (Morogoro), Mpanda Stars ya Mpanda (Rukwa), Mwadui FC (Shinyanga), Nangwa VTC (Manyara), Ndanda FC (Mtwara), Pamba SC (Mwanza), Polisi Mara (Mara), Red Coast ya Kinondoni (Dar es Salaam), Super Star ya Bagamoyo (Pwani), Tenende SC (Mbeya) na Tessema FC ya Temeke (Dar es Salaam).

No comments:

Post a Comment