- MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, May 22, 2012

Simba kuteka jiji kwa sherehe za ubingwa
Na Asha Kigundula
UONGOZI wa klabu ya Simba umesema baada ya kumalizika kwa msiba wa mchezaji wao, Patrick Mafisango, wanatarajia kufanya sherehe ya ubingwa wa Ligi Kuu walioupata msimu huu katika Ukumbi wa Dar Live Mei 27.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema wachezaji wa klabu hiyo watakuwa kwenye gari la wazi wakiwa na kombe la ubingwa wa Ligi Kuu ambalo wamelipata wiki tatu zilizopita.
Kamwaga alisema safari hiyo itaishia Mbagala kwenye Ukumbi wa Dar Live, ambapo mashabiki watapata nafasi ya kupiga picha na kombe hilo.
Alisema wameliomba Jeshi la Polisi kuwapangia barabara za kupita ili kila mmoja wao aweze kupata nafasi ya kushuhudia kombe hilo.
Katika ukumbi huo, Simba itakuwa na nafasi ya kuwaonesha pia mashujaa wa zamani walioilrtea sifa klabu hiyo, wakati pia kukiwa na tuzo maalum kwa ajili ya kiungo wao Mafisango, ambaye alifariki na kuzikwa mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Kinshasa (DRC).
"Tutakuwa na muda wa kumkumbuka Mafisango, tutatoa ngao maalum kwa ajili yake, na pia Watanzania na mashabiki wa Simba watapata fulsa ya kuangalia baadhi ya michezo ambayo alicheza akiwa na klabu hiyo, na hata video ya mazishi yake," aliongeza.
Naye nahodha wa Simba, Juma Kaseja, amewataka wana-Simba kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kushuhudia sherehe hizo na kumkumbuka shujaa wao, Mafisango.
"Ni jambo la kihistoria kuona nasi tunaweza kuwa pamoja na mashabiki wetu kwa ajili ya kuwaonesha kile tulichokivuna, nawasihi waje kwani kuna mengi ya kuangalia siku hiyo," alisema Kaseja, ambaye pia ni kipa wa timu ya taifa (Taifa Stars).
Kwa upande wake, Meneja wa Ukumbi wa Dar Live, Juma Mbizo, alisema kila kitu kinakwenda sawa, huku burudani kutoka kwa Msondo Ngoma, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Young Dee na vikundi vya sarakasi na ngoma za asili vikitarajia kunogesha.
Matembezi ya kombe hilo kuelekea katika Ukumbi wa Dar Live yataanza saa 4 asubuhi mpaka saa 10 alasiri, na kufikishwa sehemu maalum ambayo imepangwa.

No comments:

Post a Comment