- MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, May 22, 2012

Twiga Stars kuifuata Ethiopia kesho
Na Asha Kigundula
KIKOSI cha wachezaji 20 na viongozi watano cha timu ya soka ya taifa ya Wanawake (Twiga Stars), kinaondoka nchini kesho kwenda Ethiopia kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya timu ya Taifa ya nchi hiyo utakaofanyika Mei 27.

Timu ya taifa ya Wanawake Twiga Stars wakishangilia goli katika moja ya michezo yao
 Mchezo huo wa mchujo wa kuwania tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Ethiopia, utafanyika jijini Addis Ababa mwishoni mwa wiki hii.
 Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema kikosi hicho kilichopo chini ya Kocha Mkuu, Charles Mkwasa, kinaendelea na kambi yake ya kujiandaa na mchezo huo.
Wambura alisema maandalizi ya safari hiyo yanaendelea vizuri ikiwa ni pamoja na kambi ya wachezaji wa timu hiyo, licha ya kushindwa kupata majibu ya beki na nahodha wake, Sophia Mwasikili.

Wachezaji wa timu ya Taifa Twiga Stars wakiwa na nyuso za furaha baada ya kupata ushindi katika moja ya michezo yao.
 Mwasikili yuko nchini Uturuki anakocheza soka ya kulipwa, na TFF inaendeleza jitihada za kumuombea ruhusa katika klabu yake ya Daraja la Kwanza.
Twiga Stars ilicheza mechi mbili za kujipima nguvu kabla ya kwenda kuivaa timu hiyo.
Katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Zimbabwe, Twiga Stars ilipata kipigo cha mabao 4-2, wakati mechi yao ya pili dhidi ya Afrika Kusini, ilipata kichapo cha mabao 5-2, ambapo mecho zote zilifanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment