Na Hamisi Magendela
BENDI kongwe nchini iliyoanzishwa mwaka 1964 Msondo Ngoma inatarajiwa kuzindua Ukumbi wa kisasa wilayani Msasani.
Akizungimza na Jambo Leo Dar es Salaam jana Ofisa Habari wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' alisema katika uzinduzi wa ukumbi huo unaoitwa na Emirate, nyimbo za zamani zitapewa kipaumbele.
Baadhi ya wanamuziki wa Msondo Ngoma wakiwajibika jukwaani |
"Tumejiandaa vyema kufanya vizuri kama ilivo kawaida yetu katika matamasha mengi kujizolea mashabiki lukuki kutokana na mpangilio wa muziki wetu," alisema Super D.
Super D, alisema katika onesho hilo litaongozwa na kiongozi wa bendi hiyo Maalim Ngulumo baada ya afya kutengemaa vizuri na kurudi kenye jukwaa sambamba na wanamuziki wengine.
No comments:
Post a Comment