- MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, May 22, 2012

Super Cup yaandaliwa kuibua vipaji
Na Charity James
UONGOZI wa Chama cha Mpira wa Wavu Mkoa wa Dar es Salaam (DAREVA), umesema umeandaa mashindano makubwa ya mchezo huo kwa ajili ya kusaka bingwa wa mkoa yatakayojulikana kama Super Cup.
Akizungumza na Magendela Blog Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Dareva, Yusufu Mkalambati, alisema mashindano hayo yatashirikisha timu za sekondari za Dar es Salaam.
Alisema mashindano hayo yanalenga kuibua na kukuza vipaji vya wachezaji wachanga, na yamepangwa kufanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya Makongo.
"Tumeandaa mashindano makubwa ya wavu ambayo yanashirikisha shule za Sekondari zilizopo Dar es Salaam, tunatarajia yataanza siku za hivi karibuni," alisema Mkalambati.
Alisema uongozi umeshaanza kutoa fomu za ushiriki kwa waombaji, na umewataka walimu wa mchezo huo kujitokeza kwa wingi ili waziwezeshe timu za shule zao kuwania kinyang'anyiro hicho na kukuza vipaji.
Mkalambati, aliongeza kuwa hii ni mara ya kwanza kwa Dareva kuandaa mashindano hayo, ambayo lengo ni kutaka kuhamasisha mchezo wa mpira wa wavu ambao kwa siku za hivi karibuni umeanza kupata mashabiki wengi.
Kwa mshindi wa kwanza katika mashindano hayo atapata zawadi nono ikiwa ni pamoja na kikombe kikubwa na pesa taslimu ambazo hata hivyo hakuzitaja kiasi chake, sambamba na vyeti kwa washiriki.

No comments:

Post a Comment