- MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, May 22, 2012

TLGU kuita timu ya mashindano ya Chalenji
Na Asmah Mokiwa
CHAMA cha Gofu cha Wanawake Tanzania (TLGU), kinatarajia kutangaza kikosi cha wachezaji watatu watakaoingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya Chalenji, yanayotarajia kufanyika Juni mwaka huu nchini Botswana.
Akizungumza na Magendela Blog  Dar es Salaam jana, Rais wa TLGU, Mbonile Barton, alisema kikosi hicho kitatangazwa wiki hii, ambacho kitaanza rasmi mazoezi na kuweka kambi ya pamoja.
Kwa mujibu wa Mbonile, miongoni mwa wachezaji watakaounda kikosi hicho ni wale walioipa nchi ushindi katika mashindano ya Afrika Mashariki na Kati yaliyofanyika hivi karibuni hapa nchini.
Alisema wachezaji hao watakaochaguliwa ni moja kati ya wale walioweza pia kuliwakilisha vyema taifa katika mashindano ya gofu, hivyo wataingia kambini mapema ili kujiandaa na mashindano hayo ya kimataifa.
"Kwa sasa, wachezaji hao wanaendelea na mazoezi makali kwa kila mmoja katika kambi yake, na hata mchezaji mmoja aliyekuwa nje atawasili nchini Mei 24 kwa ajili ya kujiunga na wenzake kuanza kwa kambi hiyo ya pamoja," alisema Mbonile.
Alisema, wameamua kambi hiyo iwe Dar es Salaam kutokana na wadhamini kuwepo mkoani humo, ambapo wameamua kubadilisha mahali pa kuweka kambi hiyo, wakati awali walipanga kuifanyia Arusha.

No comments:

Post a Comment