Na Asha Kigundula
UONGOZI wa klabu ya Simba umempa mkataba wa miaka miwili Kocha Mkuu wa timu hiyo, Milovan Cirkovic, baada ya kupenda utendaji wake.
Habari kutoka ndani ya klabu hizo zinasema kuwa Milovan ambaye alipewa mkataba wa miezi sita, amepewa mkataba wa miaka miwili ambao umeanza rasmi wiki hii.
Chanzo hicho kimesema kocha huyo ambaye anatarajia kwenda mapumziko nchini Serbia, ameshakabidhi ripoti yake kwa Kamati ya Usajili.
Kimesema kuwa katika ripoti hiyo kocha Cirkovic, ameitaka kamati hiyo isajili nafasi ya ulinzi na kiuongo mkabaji.
Chanzo hicho kimesema Cirkovic ameitaka kamati hiyo kusajili wachezaji toka nje ya nchi kutokana na mchango wao mkubwa katika timu hiyo.
![]() |
Milovan Circovic, Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Simba ambao ni mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara . |
Chanzo kimesema tayari kimeanza kuyafanyia kazi maombi hayo ambapo tayari kamati za Ufundi na Usajili zimeshakutana kujadili ripoti hiyo.
Kimesema kuwa tayari wachezaji wawili Derreck Walulya na Gervas Kago tayari wameshamaliza mikataba yao na haitaongezwa.
Wachezaji hao tayari wameshamalizana na Simba kwa kuwa mikataba yao imeisha na kutokana na mchango wao mdogo katika timu hiyo wameamua kuwaacha katika usajili ujao.
Wakati huo huo, klabu ya Simba, jana imemaliza maombolezo ya mchezaji wao, Patrick Mafisango, aliyefariki dunia Alhamisi iliyopita kwa ajari ya gari.
cioo
TFF yambeba Nchunga
- Yadai hawatambui mapinduzi yao
Na Asha Kigundula
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limesema halitambui mapinduzi yaliyofanywa na wanachama wa klabu ya Yanga, ikiwataka kuangalia katiba.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, alisema kuwa TFF bado inatambua uongozi wa Lloyd Nchunga, nasi si ya muda ambayo ilitangazwa juzi kwenye mkutano wa dhalura wa wanachama.
Osiah, alisema msimamo wa TFF kwa wanachama wake hauna budi kuheshimiwa hivyo hakuna uongozi wa kamati ya muda kama ulivyotangazwa juzi.
Alisema mara baada ya kusikia kuna migogoro ndani ya kjlabu hiyo walkimuhita nchunga na kuongea nae hivyo wanachama wanatakiwa kusubili muda wa mkutano mkuu ambao ni Julai 15.
"Hatuwezi tukaruhusu mambo kama haya katiba ni lazima iheshimiwe hivyo basi hakuna maamuzi yanayoweza kutolewa bila ya kamati ya utendaji kukaa na kuyapitisha.
Osiah alisema kuwa Seketarieti ya TFF ilipokaa na Nchunga ilimwambia wakutane pande zote mbili na kuondoa tofauti zao kabla ya mkutano mkuu.
Alisema hata kama kiongozi atakiwi na ana matatizo ni lazima wafuate utaratibu lakini si kufanya mkutano usio halali.
"Kama kiongozi atakiwi ni lazima afuate utalatibu na si kufanya mapinduzi ambayo hayakubaliki, TFF hatuwezi kufanya kazi na kamati ya kuteuliwa ambayo haikufauata katiba...waangalie katiba kwanza"alisema Osiah.
![]() |
Angetile Osiah katibu mkuu wa TFF |
Kipengele cha (3) kinasema wito wa mkutano unatakiwa utolewe angalau siku 15 kabla ya mkutano wakati kipengele cha (4) kinasema ajenda, nyaraka muhimu zipelekwe kwa wanachama siku saba kabla ya mkutano.
Osiah alisema endapo kuna wajumbe wamejiuzulu mkutano mkuu unakuja unawezo wa kuchagua wengine kuziba pengo la walijiuzulu au kufanya uchaguzi wa kuziba nafasi hizo.
"Endapo kama kuna wajumbe wa kamati ya utendaji wamejiuzulu unaweza ukafanyika uchaguzi wa kuziba nafasi hizo..wakae chini na kupatikana muhafaka suala la uongozi wa kamati ya muda kwetu halipo"alisema Osiah.
Juzi wanachama wa Yanga walifanya mkutano wa dharura ambao ulitangaza kumvua Nchunga na kamati ya utendaji.
ciooo
No comments:
Post a Comment