Na Asha Kigundula
KIKOSI cha timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) kinawasili nchini kesho kutwa kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya timu ya Taifa (Taifa Stars) utakaofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah, alisema kuwa wameshapata taarifa ya ujio wa wageni wao (Malawi).
Alisema licha ya kujua siku ya kuja, lakini bado hawajataja idadi ya watakaokuja licha ya TFF kuwapa idadi ya watu 27, ambao watakuwa chini yao.
"Tumewaambia wakija 27 ni idadi ambayo itakuwa chini yetu kama watazidi wengine watakuwa chini ya Chama cha Mpira wa Miguu Malawi," alisema Osiah.
Stars iliyopo kambini chini ya kocha Kim Poulsen, inacheza mechi kwa ajili ya kujipima nguvu kabla ya kwenda kuivaa timu ya taifa ya Ivory Coast ugenini Juni 2, jijini Abidjan.
Mechi hiyo ya mchujo wa kuwania tiketi ya fainali za Kombe la Dunia 2014 kwa kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast.
Wachezaji ambao wapo kambini kujiandaa na mchezo huo makipa; Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally (Azam) na Deogratius Munishi (Mtibwa Sugar).
Mabeki: Nassor Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Simba), Waziri Salum (Azam), Shomari Kapombe (Simba) na Juma Nyoso (Simba).
Viungo ni Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum Abubakar (Azam), Nurdin Bakari (Yanga), Jonas Mkude (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Edward Christopher (Simba- U20), Mrisho Ngasa (Azam) na Frank Domayo (JKT Ruvu- U20).
Washambuliaji ni Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Ramadhan Singano (Simba-U20), Simon Msuva (Moro United- U20), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo), Haruna Moshi (Simba) na John Bocco (Azam).
ccuoo
Samata, Ulimwengu kujiunga Stars kesho
Na Asha Kigundula
WACHEZAJI wa timu ya soka ya Taifa (Taifa Stars) Mbwana Samata, Thomas Ulimwengu na Haruna Moshi 'Boban' wataungana na wenzao katika kambi ya timu hiyo kesho.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisemawachezaji Samata na Ulimwengu wanajiunga katika kambi hiyo wakitokea nchini Congo katika timu yao ya TP Mazembe, ambayo wanaichezea.
![]() |
Mbwana Samatta |
Wambura, alisema kuwa Samata na Ulimwengu watawasili nchini saa 1 asubuhi, wakati Boban amewasili jana, lakini ataanza mazoezi na kambi leo pamoja na wenzake hao.
![]() |
Haruna Moshi 'Boban' |
Kabla ya mchezo huo, Stars itakuwa na mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Malawi, itakayofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumamosi.
cuoo
Kesi ya Lulu yaendelea kurushwa
Na Grace Gurisha
KESI ya mauaji inayomkabili msanii wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu', imehairishwa hadi Juni 4 mwaka huu kwa sababu upelelezi bado haujakamilika.
Shauri hilo lilikuja jana mbele ya Hakimu, Agustina Mmbando, wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, ambapo kesi hiyo ilikuja kwa kutajwa.
Wakili wa Serikali, Ladslaus Komanya, alidai kuwa kesi hiyo imekuja kwa kutajwa wanaomba tarehe nyingine ya kutajwa na upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika. Upande wa utetezi alikuwepo wakili Peter Kibatala na Masawe.
Kutokana na upelelezi kutokamilika, Mmbando aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 4 mwaka huu, ambapo itakuja kwa kutajwa.
Mara ya mwisho kesi hiyo ilipofika kwa ajili ya kutajwa, Mei 7, mahakama ilitupilia mbali ombi la mawakili wa upande wa utetezi katika kesi inayomkabili Lulu kuwa mahakama imuone ana miaka
chini ya miaka18.
Baada ya mahakama hiyo kutupilia mbali, upande wa utetezi wamepeleka ombi hilo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.Ombi hilo litasikilizwa na Jaji Dk. Fauz Twaibu wa mahakama hiyo
Mei 28 mwaka huu. Lulu anatuhumiwa kwa mauaji ya nguli wa
filamu nchini, Steven Kanumba.
No comments:
Post a Comment