DIAMOND KUPIGA SHOO BBA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, October 5, 2014

DIAMOND KUPIGA SHOO BBA


Nasseb Abdul ‘Diamond Platnumz'.
STAA wa Bongo Fleva nchini, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz' leo anatarajiwa kupiga shoo ya nguvu kwenye ufunguzi rasmi wa shindano la Big Brother Afrika 2014, nchini Afrika Kusini.
Diamond anatarajiwa kupamba shoo hiyo ya ufunguzi ambapo pia atakuwa sambamba na mwanamuziki wa Nigeria, Davido watakapoimba wimbo wao wa ‘Number One Remix’.
Hii ni mara ya pili kwa Diamond kupiga shoo katika ufunguzi wa shindano hilo la BBA, awali alifanya hivyo katika msimu wa saba.
Shindano hilo la kila mwaka, linaloandaliwa na kampuni ya Multchoice, msimu huu ni la 9, likijulikana kama ‘Big Brother Hotshots’ linashirikisha washiriki kutoka nchi 12 za bara la Afrika na mshindi anatarajiwa kuondoka na kitita cha dola 300,000.BBC

No comments:

Post a Comment