MWIGIZAJI wa kike Aunty Ezakiel amemzodoa msanii wa kizazi kipya Harmo Rappa kwa kusema kuwa hama kipaji cha kufanya muziki huo kutokana na kutumia nguvu nyingi katika kujiweka katika chati za juu kwenye tasnia hiyo.
Hayo aliyasema wiki hii wakati akijibu maswali ya maswali ya mashabiki kupitia mtandao wa kijamii 'Facebook' wa EATV katika kipindi cha Kikaangoni, Aunty alisema rapper huyo anatumia nguvu nyingi kuliko uwezo wake katika kujitangaza ingawa hana kipaji muziki.
“Simkubali Harmo Rappa maana hana kipaji cha muziki kwani anatumia nguvu nyingi kujiweka katika chati za tasnia ya muziki huu ,” alisema.
Hata hivyo Harmo amemchana Mose Iyobo ambaye ni mzazi mwenzake na Aunty katika wimbo wake mpya ‘Kiboko ya Mabishoo’ aliomshirikisha mkongwe wa muziki huo Juma Kassim 'Sir Juma Nature'.
No comments:
Post a Comment